jaribio_la_2

Mbao FC ipo tayari kuwakabili Singida United


Kikosi cha Mbao Fc kipo katika maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mechi ya raundi ya pili na tatu ya ligi kuu ya vidacom. Timu ya mbao Fc inatarajiwa kucheza na Singida United siku ya jumapili tarehe 10.9.2017 kabla ya kuelekea morogoro kucheza na mtibwa wiki inayofuata.
Kwa muda wa miezi miwili sasa kikosi cha mbao Fc kimekuwa kambini katika chuo cha ualimu Butimba Mwanza kikijiweka tayari kwa michezo ya ligi kuu.
Katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya kagera  mbao Fc ilifanikiwa kuvuna point tatu muhimu kwa ushindi wa goli moja. Goli la mbao Fc lilifungwa na mchezaji wa timu ya taifa Boniface Maganga.

No comments

Powered by Blogger.