jaribio_la_2

Kampuni ya Jambo Food Products yatoa msaada wa maji kwa Mbao Fc


Kampuni ya Jambo Food Products yenye Makao yake Shinyanga na Mwanza, imetoa msaada wa maji kwa timu ya mbao Fc kwa kipindi chote cha smimu wa ligi uliosalia.

Akizungumza na mbaofc.blogSpot.com meneja masoko wa Jambo Food Products Ndugu Johnson Mchuma alisema msaada huo unajumuisha mambo yafuatayo:
  • Msaada wa cartons 11 za maji ya lita moja na nusu kwa siku kwa kipindi chote cha ligi
  • msaada wa kujenga mgahawa wa kisasa katika eneo la saba saba ilipo maskani ya mbao Fc. Mgahawa huu mbali na kuwa na kuuza chakula na vinywaji, utakuwa pia na eneo maalumu la kuoneshea mpira ambapo mashabiki wa Mbao Fc watapata fursa ya kutazama mpira pindi timu yao itakapokuwa inacheza ugenini.
  • msaada wa vinywaji na juisi pindi timu itakapokuwa inafanya shughuli za kijamii.
Akizungumza na mbaofc.BlogSpot.com, mwenyekiti wa Mbao Fc ndugu Soly Zephania Njashi alisema; "huu ni msaada mkubwa sana kwa timu na ni hatua muhimu sana kuelekea udhamini kamili. Ni imani yangu kuwa katika kipindi kijacho Jambo Food Products watafikia uamuzi wa kuipa Mbao Fc udhamini wa moja kwa moja"

Naye katibu wa mbao Fc Ndugu Daniel Naila alisema kuwa msaada huu ni muhimu sana kwani unapunguza gharama za uendeshaji wa timu kwa kiasi kikubwa.

No comments

Powered by Blogger.