jaribio_la_2

Kuelekea Mechi ya Simba: Kikosi cha Mbao Fc kipo tayari


Kikosi cha timu ya Mbao Fc jana kimeendelea na mazoezi katika viwanja vya chuo cha ualimu butimba ikiwa ni muendelezo wa maandalizi ya mechi ijayo ya alhamisi dhidi ya Simba. Akizungumza na mbaofctz.BlogSpot.com, kocha mkuu wa Mbao Fc alisema kuwa ameandaa kikosi chake tayari kwa changamoto ya mechi nne za nyumbani zinazokuja
"Tupo tayari kwa mechi zijazo. Sio mechi ya samba tuu. kwetu sisi kila mechi ni fainali na tutajitahidi kufanya vizuri kwa kila mechi iliyopo mbele yetu"
 
Mechi tatu Point Tatu
Katika michezo mitatu ya iliyopita Mbao Fc imefanikiwa kukusanya point tatu. Mechi zote zilichezwa ugenini. Mbao Fc ilianza kwa Kuifunga Kagera goli moja bila kabla ya kupoteza kwa magoli mawili kwa moja dhidi ya Singida United na Mtibwa.
 
Maendeleo Kulinganisha na Msimu Uliopita
Kikosi cha Mbao Fc kinaelekea kuimarika ukilinganisha na msimu uliopita kipindi kama hiki.
baada ya mechi tatu msimu uliopita mbao fc ilikuwa imefanikiwa kukusanya point 1 baada ya mechi moja ugenini na mechi mbili za nyumbani.
 
Historia ipoje Mbao Fc inapocheza dhidi ya simba?
Katika msimu uliopita Mbao Fc ilicheza mechi tatu dhidi ya samba na kupoteza zote ikiwamo mechi ya fainali ya kombe la FA ambapo Mbao Fc ilipoteza kwa taabu baada ya ya mchezo wa dakika 120.
 

No comments

Powered by Blogger.