Mbao Fc Tayari Kuwavaa Mtibwa Kesho
Kikosi cha Mbao Fc Kimewasili salama Manungu Morogoro kwa ajili ya mchezo wa raundi ya tatu ya ligi kuu ya Vodacom. Katika mchezo uliopita kikosi cha mbao fc kilipoteza kwa magoli mawili kwa moja dhidi ya Singida United.
Kwa mujibu wa benchi la ufundi, kikosi kipo tayari na hakina majeruhi yoyote aliyeongezeka ukiachilia majeruhi walioachwa kambini mwanza kwa matibabu. Baada ya nchezo wa wa kesho kikosi kitasafiri kuja mwanza tayari kwa mawindo ya mechi dhidi ya samba itakayofanyika tarehe 21.9.2017 katika uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza.


No comments